Monday, November 19, 2012
RC AAGIZA MAZAO YAFYEKWE ILI KUNUSURU MIGOGORO TARIME *asema mipaka ionyeshwe vizuri *wananchi wataka Serikali kuwekeza eneo hilo
KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA MKOA
WA MARA,IMELIAGIZA JESHI LA KUJENGA TAIFA JKT KWA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA
POLISI,KUTEKETEZA MAZAO YOTE AMBAYO YAMEPANDWA KATIKA MASHAMBA YENYE UKUBWA WA
HEKTA 193.3 IKIWA NI NJIA MOJA WAPO YA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI KATIKA KATA
MBILI ZA WILAYANI TARIME.
SERIKALI LITWAA ENEO HILO MIAKA
KADHAA ILIYOPITA BAADA YA KUGOMBANIWA NA WANANCHI KWAAJILI YA KILIMO JAMBO
AMBALO LIMEKUWA LIKISABABISHA MAPIGANO YA KOO YA MARA KWA MARA NA
KUSABABISHA MAUJI YA WANANCHI.
MWENYEKITI WA KAMATI HIYO,AMBAYE PIA
NI MKUU WA MKOA WA MARA BW JOHN GABRIEL TUPPA,AMETOA AGIZO HILO,BAADA YA
KUTEMBELEA ENEO HILO NA KUKUTA LIKIWA LIMELIMWA MAZAO MBALIMBALI YAKIWEMO
MAHINDI HATUA AMBAYO SASA IMEANZA KUONYESHA VIASHIRIA VYA KUTOKEA KWA MAPIGANO
YA KOO ZA WANCHARI NA WAKIRA KUTOKA KATA ZA MWEMA NA NYAMARAGA KATIKA WILAYA
HIYO YA TARIME.
AIDHA MKUU HUYO WA MKOA WA
MARA,PAMOJA NA KUVIAGIZA VYOMBO HIVYO VYA ULINZI NA USALAMA KUYATAIFISHA NA
KUYATEKETEZA MAZAO HAYO PIA AMEAGIZA KUKAMATWA WATU AMBAO WANAHUSIKA KUFYEKA
ZAIDI YA EKARI 100 ZA MAZAO MBALIMBALI MASHAMBANI PAMOJA NA KUSABABISHA KIFO
CHA ROBERT CHACHA MARWA AMBAYE ALIFARIKI BAADA YA KUKATWAKATWA NA MAPANGA AKIWA
SHAMBANI
KWA MUJIBU WA MKUU WA MKOA WA
MARA,ENEO HILO SASA LITAKUWA CHINI UANGALIZI WA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWAAJILI
YA SHUGHULI MBALIMBALI ZITAKAZOPANGWA NA JESHI HILO KUANZIA SASA,HUKU VIONGOZI
NA WATENDAJI WA WILAYA NA MKOA WAKIAGIZWA KUPIMA UPYA MIPAKA YA VIJIJI HIVYO.
Saturday, November 3, 2012
HARAMBEE YA KUCHANGIA KANISA KUU LA PAROKIA MPYA YA UTEGI
Katika Harambee hiyo zaidi ya Shilingi Milioni 35
zilipatikana huku Mifugo kama Mbuzi na Ng’ombe zikitolewa piambali na hivyo
Vifaa vya Ujenzi Vilitolewa katika Harambee hiyo huku Mbunge wa Jimbo hilo
Lameck Airo na Diwani wa Kata ya Roche Mh Ochele wakisema kuwa katika uchaguzi
mkuu ujao hawatagombea tena katika nafasi hizo
Mbunge wa jimbo la Rorya Mh Lameck Airo Kulia akiwa na Diwani wa kata ya Roche Mh Ochele ambapo kwa pamoja wamesema hawatagombea tena katika nafasi hizo mwaka 2015
Mbunge wa Rorya awatoa machozi
waumini wa kanisa katoliki baada ya kutangaza kutogombea tena ubunge
Na Mwandishi wetu,Rorya
Mbunge wa
jimbo la Rorya mkoani Mara Lameck Airo,juzi alisababisha waumini wa kanisa katoliki
parokia mpya ya Utegi na mamia ya wananchi walikuwa kanisani hapo,kuangua vilio
baada ya kutangaza kung’atuka katika siasa na kwamba hawezi kugombea tena
ubunge.
Kwa sababu
hiyo mbunge huyo,alisema pamoja na kuacha siasa na kuacha kugombea ubunge,lakini
atazidi kuwa mwanachama mwaminifu wa ccm kwa kushirikiana na wenzake katika
kuhakikisha kinashinda katika chaguzi mbalimbali zijazo.
Mwenyekiti
wa halmashauri ya Rorya Charles Ochele,ndio alianza kuwafanya waumini hao kuwa
katika nyuso za uzuni na wengine kububujikwa na machozi baada ya kuitwa na
mbunge huyo kwaajili ya kuchangia ujenzi wa kanisa kuu la parokia ya Utegi.
Kabla ya
kutoa mchango wake wa mifuko 100 ya saruji na kiasi cha milioni sita,Ochele
ambaye ni diwani wa CCM kata ya Roche, alisema wameamua kusitaafu siasa na sasa
nguvu zinaelekezwa katika kuchangia nyumba za ibada.
“Nimekuja
kumuunga mkono mbunge wangu kuijenga hii nyumba ya mungu,lakini leo naona
wachangiaji ni wachache tofauti na kule kwenye siasa ambao wamekuwa wakitoa
fedha nyingi kutafuta vyeo ndio maana mimi na mbunge wenu tumetangaza siasa
basi kwani kuna watu wamefika hadi kutusema vibaya kwa tamaa tu ya vyeo hivyo
tunawapisha nao waweza kusaidia maendeleo yetu”alisema na kuongeza.
“Tunaacha
siasa tukiwa tumeweka msingi mzuri katika jimbo la Rorya na sasa nguvu zetu
tunazihamishia katika nyumba za ibada kwani tukifanya hivyo tutazidi
kuhimalisha amani katika jimbo letu baada ya wananchi kupata neon la mungu”alisema
Ochele huku wananchi na waumini hao wakibubujikwa na machozi.
Hata hivyo
baada ya kukabidhi mchango huo nakumpa kisemeo mbunge huyo,Airo aliwaambia mamia
ya waumini na wananchi hao ndani ya kanisa hilo kuwa tayari ametangaza
kutogombea ubunge mwaka 2015 ili kutoa nafasi kwa wananchi wengine wa wilaya ya
Rorya kupokea kijiti hicho kauli ambayo ilionekana kupingwa na wananchi huku
wengi wakionyesha nyuso za uzuni.
“Nilitangaza
nataka nifanye ubunge kwa miaka mitano ili niweze kutoa mchango wangu na baada
ya hapo sitagombea tena ubunge nastaafu siasa kwaajili ya kukaa na familia
yangu hatua ambayo nitatoa nafasi kwa mwenzangu kuendeleza hapa
nilipofikia”alisema Airo.
Alisema
katika moja ya vikao vya halmashauri kuu ya ccm,alitangaza uamuzi wake huo
baada pia kuchukizwa na baadhi ya wanasiasa kubaguana,kutompa ushirikiano
katika utekelezaji wa miradi huku wengi wakipinga hatua yake ya kutekeleza
miradi ya maendeleo katika jimbo zima bila kubagua kata za wapinzani.
Akizungumzia
ujenzi wa kanisa hilo,alisema alikubali kuongoza harambee hiyo baada ya
kuridhishwa na mchango mkubwa wa madhehebu ya dini katika kusaidia sekta
mbalimbali za maendeleo katika jimbo hilo.
Alisema viongozi
wa dini wana kila sababu ya kupongezwa kwa jinsi walivyosadia kurejesha amani
katika wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na kukemea vitendo vya wizi wa
mifugo,uporaji,ubakaji na matumizi ya dawa za kulevya ambavyo alidai vilichangia
kudhorotesha hali ya amani katika wilaya ya Rorya.
“Napenda
kuwapongeza sana viongozi wa dini hasa kanisa hili jinsi lilivyosaidia sekta za
maji,afya,nishati ya umeme,kilimo na ufugaji katika jimbo letu jambo ambalo
limesaidia kwa kiasi kikubwa kuharakisha maendeleoo ya wananchi wetu na wilaya
yetu kwa ujumla”alisema Airo.
Awali paroko
wa parokia mpya ya Utegi Padri Benedict Luzangi,limewaomba viongozi wa dini
kuepuka kutumia nyumba za ibada kutoa kauli za uchochezi zinazolenga kulipiza
kisasi dhidi ya dini na dini nyingine ikiwa ni njia moja wapo ya kulinda amani
na utulivu uliopo nchini.
Alitoa kauli
hiyo wakati akitoa mahubili kabla ya kufanyika kwa harambee ya kuchangia ujenzi
wa kanisa kuu la parokia hiyo katika mji mdogo wa Utegi wilayani Rorya.
Alisema kuna
baadhi ya watu wamekuwa wakitumia nyumba za ibada na mgongo ya dini zao kutoa
kauli za uchochezi vitendo ambavyo amesema hakuna dini inayoruhusu kufanya
hivyo bali watu hao wanapaswa kuhukumiwa kwa matendo yao badala ya kuhusisha
dini nzima na matendo hayo mauvu ambayo kwamwe hayawezi kumpendeza Mungu.
Kuhusu
vurugu na matukio ya hivi karibuni ambayo yamekuwa yakihusisha baadhi ya watu
wakitumia kivuli cha dini,kiongozi huyo wa kanisa katoliki amesema kamwe
matukio hayo yasihusishwe na dini nzima bali vyombo vya dola vinapaswa
kuwashughulikia kama wahuni ambao wanataka kutumia dini kuvuruga amani ya nchi.
Katika
harambee kiasi cha shilingi milioni 35 kilipatikana ikivikiwemo vifaa vya
ujenzi,mifugo kama vile ng’ombe na mbuzi
huku mbunge huyo akichangia kiasi cha shilingi milioni tano.
MBUNGE WA JIMBO LA RORYA KATIKA ZIARA YAKE YA KUTEMBELEA MIRADI ALIYOIJENGA KWA UFADHILI WAKE
Mh Lameck Airo Mbunge wa Jimbo la Rorya akikagua Daraja lililojengwa kwa Ufadhili wake jimboni humo
Moja ya jengo la Walimu alilolijenga katika Mh Lameck Airo,ambapo yote mawili yaligharimu kiasi cha Milioni 26
Mh Lameck Airo akipata Maelekzo
Watoto wa shule ya Msingi Utegi wakipata Mlo shuleni hapo
Ukaguzi ukiendelea katika Daraja
Moja ya Nyumba ya Walimu iliyojengwa na Mh Airo
Mh Lameck Airo akiweka saini katika kitabu cha Kumbukumbu
Mh alitupia maneno kidogo
Usikuvu ulikuwa 100 kwa 100
Moja ya jengo la Walimu alilolijenga katika Mh Lameck Airo,ambapo yote mawili yaligharimu kiasi cha Milioni 26
Mh Lameck Airo akipata Maelekzo
Watoto wa shule ya Msingi Utegi wakipata Mlo shuleni hapo
Ukaguzi ukiendelea katika Daraja
Moja ya Nyumba ya Walimu iliyojengwa na Mh Airo
Mh Lameck Airo akiweka saini katika kitabu cha Kumbukumbu
Mh alitupia maneno kidogo
Usikuvu ulikuwa 100 kwa 100
Subscribe to:
Posts (Atom)