MPWA WA GEORGE MARATO AKITIMIZA MOJA YA MILA ZA KIKURYA,PICHA 30 ZA TOHARA KATIKA KIJIJI CHA RYAMISANGA, PART 1
*Picha 30 za sherehe ya Mpwa wake na Mwandishi wa habari wa ITV & Redio one mkoani Mara George Marato,Mkazi wa kijiji cha Ryamisanga wilaya ya Butiama Mkoani Mara.Taarifa zinasema kuwa kwa mila ya Kabila ya Kikurya unapokaribia kutimiza Umri wa utu uzima lazima utairiwe na hivyo kuruhusiwa kuingia katika Mapenzi na kushiriki katika Tambiko zote za Kimila.
*Lakini pamoja na kutimiza moja ya mila katika kabila hilo lakini pia wataalamu wa Afya wanasema kuwa mtu anapotairiwa ana zaidi ya asilimia 60 kujikinga na magonjwa Mbalimbali ukiwemo Ugonjwa wa Ukimwi,kufuatia hatua hiyo Serikali ya Tanzania iliamua kufanya zoezi hilo la kutairi baadhi ya Mikoa hapa Tanzania ukiwemo mkoa wa Mara katika wilya ya Rorya* Matukio yote utayapata kupitia blog hii ya Mwana wa Afrika na hapa ni Part 1
Umati mkubwa wa watu wakicheza ngoma ya kikurya "Maarufu kama LITUNGU kabla ya tohara kufanyika
Marato yupo kati akimwaga noti kwa kijana kwa kuonyesha ujasiri wa kukubali kutimiza mila ya kabila yao
Noti bado zinaendeleee kumiminwa
Baada ya kutoa noti jamaa akaingia kati kucheza ngoma
Dogo bado anachemsha damu kwa kucheza ngoma ya Kikurya
Akina mama hawapo nyuma katika kusherekea sherehe hiyo
Huyu jamaa anayepiga lilandi cjui akitoaka hapo Msosi utasalimika
Kushoto Mwana wa Afrika kuli Shommy B tuliamua kumuunga Mkono Kijana
Noti zaendelea kumiminika
Shommy B akiwa ameshika kitu,cjui nininin?
Maria Marato kushoto na Marato kulia wakiwa na ndugu yao ambaye jana ametimiza Moja ya Mila za Kikurya
Hawa Jamaa waliishatimiza hiyo mila na hapa wanamtazama Mwenzao kama atalia au vp
Marato kama vile aamini kama mdogo atavumilia kisu kukamilisha Moja ya mila ya Kabila lao
Jamaaa wana Mbwembwe hawaaaaaaaaaaaaa
Dakika ya Mwisho kabisa kabla ya Kisu Marato akarudi tena na kuanza kutoa Msimbazi kibao
Du muda ukawadia, huyu jamaa anayevaa groves tayari kwa kumaliza kazi kwa kijana
Tayari mambo yameiva na kijana kaishatoa bukta kama ni kufa nife
Jamaa akasogea mbele ya Kijana tayari kwa kumaliza kazi
Haya sasa mambo ndyo hayo,jamaa kaanza kufanya Mambo
Endelea kuangalia Blog hii uone nn kitafuatia je kijana alilia au vp?
No comments:
Post a Comment