-Pia watumishi wa idara ya maji
Mugango,Kiabakari na Butiama wafikisha madai ya mishahara ya miezi 26 hadi
miaka mitatu
-Pia hakuna mwandishi aliyeshushwa na
Muwasa kushiriki katika ziara ya naibu waziri kama ilivyoripotiwa awali
HATIMAYE
Serikali imepanga kutekeleza mradi mkubwa wa maji katika Manispaa ya Musoma
mkoani Mara ambao unatarajia kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 41.
Naibu waziri
wa Maji Mh Mhandisi Dk Benilith Mahenge,ametoa taarifa hiyo mjini Musoma wakati
akizungumza na uongozi wa mkoa wa Mara,ambapo amesema tayari mipango wa kuanza
utekelezaji wa mradi huo mkubwa imekamilika baada ya serikali kupata fedha
kutoka nchi za Ujerumani na Ufaransa.
Amesema
mradi huo pamoja na kuchelewa kuanza utekelezaji wake kwa zaidi ya miaka
mitatu
lakini utalenga kuhamisha chanzo cha maji cha sasa na kujengwa upya
katika eneo
la Bukanga pamoja na kufufua na kuongeza miundombinu mipya ya maji ili
kukidhi hitaji la maji kwa wananchi na taasisi zote katika
Manispaa ya Musoma.
Kwa upande
wake mkuu wa mkoa wa Mara Bw John Tupa,pamoja na kupongeza hatua hiyo ya
serikali kwa kukubali kutekeleza mradi huo katika unaolenga kuwandolea kero
kubwa ya upungufu wa maji inayowakabili wananchi lakini pia ameahidi kuwa
serikali ya mkoa itahakikisha inapambana na vitendo vyote vya hujuma ambayo
inaweza kujitokeza katika utekelezaji wa mradi huo.
Wakati huo
huo baadhi ya watumishi wa serikali katika mradi wa maji wa Mugango,Kiabakari
hadi Butiama wanadai mishahara yao ya kati ya miezi 26 hadi 30 jambo ambalo
limewafanya kuishi maisha ya kuomba omba.
Wafanyakazi
hao wametoa kilio hicho baada ya naibu waziri wa Maji Mh Mhandisi Dk Binilith
Mahenge kutembelea mradi huo ambao pia umekuwa ukikabiliwa na uchakavu mkubwa
wa miundombinu ya kusambazia maji kenda kwa wananchi ikiwemo familia ya baba wa
Taifa hayati Mwl Julius Nyerere.
Wakiwa na
mabango wafanyakazi hao ambao wengi ni vibarua wa kudumu wamemueleza na naibu
waziri huyo kwa nyakati tofauti kuwa
hivi sasa baada ya kutoka kazini wanalazimika kufanya vibarua vikiwemo
vya kulima mashamba kwaajili ya kupata fedha za kuhudumia familia zao.
Kufuatia
kilio hicho,naibu waziri huyo wa maji,ameuagiza uongozi wa mamlaka ya maji ya
Mugango,Kibakari hadi Butiama,halmashauri ya Musoma na ofisi ya mkuu wa wilaya
ya Butiama kumpatia maelezo ya sababu za wafanyakazi hao kutolipwa mishahara
yao kwa kipindi hicho pamoja na kuorodhesha madai yote ambayo yanadaiwa na
watumishi hao ndani ya siku tatu.
Amesema
kushindwa kulipa mishahara hiyo kwa wakati kunaweza kuchangia watumishi wasio
waaminifu kufanya hujuma kubwa ikiwa ni pamoja na kuiba mashine za mradi huo
jambo ambalo linaweza kuingizia hasara kubwa serikali huku akitoa mwezi mmoja kwa meneja wa mradi huo
mhandisi Merchedes Tibita kuongeza ukusanyaji wa mapato ambayo yatawezesha
kutatua baadhi ya changamoto zinazoukabili mradi huo.
ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA MAJI MH ENG DK BINILITH MAHENGE WILAYA ZA MUSOMA NA BUTIAMA
Naibu waziri wa Maji Mh Dk Binilith Mahenge akiwa pamoja na DC Musoma Jackison Msome na mkurugenzi wa MUWASA Gines Kaduei
Mh Mahenge akiwa pamoja na viongozi wa wilaya ya Butiama
Meya wa Manispaa ya Musoma Alex Kisurura wa kwanza kulia akiwa na naibu waziri wa maji na viongozi wa Manispaa ya Musoma
Picha ya juu mkurugenzi wa Muwasa akimunyesha mitambo naibu waziri wa maji
Chanzo cha maji cha Muwasa katika ziwa victoria ambacho kinahitajika kuhamishwa kwa gharama ya bilioni 41 kwaajili ya kuwezesha mji wa Musoma kupata maji ya uhakika
Sehemu ya mji wa Butiama
Viongozi wa wilaya ya Butiama wakiwa na naibu waziri wa maji wa kwanza kushoto ni Magina Magesa m/kiti wa halmashauri ya Musoma
Chanzo cha maji cha mradi wa Mugango,Kiabakari hadi Butiama
Naibu waziri akiwa pamoja viongozi wa wilaya ya Butiama
Bango la wafanyakazi wa maji Mugango/Butiama ambao wanaidai serikali miezi 26 hadi miaka mitatu
Sehemu ya mji wa Butiama
Naibu waziri wa maji Mh Mahenge akisoma moja ya bango
Naibu waziri wa maji akiangalia Bwawa la Kiarano
Naibu waziri akitoa heshima katika kaburi la Baba wa taifa kijijini Butiama
Emanuel Ams wa TBC akisalimiana na mjane wa baba wa Taifa mama Maria Nyerere
Naibu waziri akisalimiana na mama Maria Nyerere
Naibu waziri akitoa neno la shukurani kwa Mama Maria Nyerere
No comments:
Post a Comment