Alisema kuteuliwa
yeye hakuna maana kuwa kuna jambo limekosewa bali ni taratibu za chama na
kwamba kwa asilimia mia moja anaunga mkono uamuzi huo ambao umefanywa katika
vikao mbalimbali vikiwemo vile vilivyokuwa chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya
Kikwete jana.
“Mimi ni mwana
ccm damu ninaunga mkono uamuzi wa chama changu tena kwa asimia mia
moja,walioteuliwa ni wanaccm wenzangu ninatoa ahadi ya kuwapa ushirikiano wa
kutosha hadi tutakapo pata mmoja wetu kuwa kiongozi wa jumuiya yetu”alisema
Mkono.
Kuhusu kauli yake
kuwa endapo hatapitishwa jina lake hapatatosha ndani ya CCM alisema kauli ile
aliitoa kwa kusema kuwa hakubaliani nay ale yaliandikwa kwenye magazeti kwa
vile kulikuwa bado kuna vikao vilikuwa vikiendelea ndani chama hicho.
“Nilisema
sikubaliani nay ale yaliandikwa kwenye magazeti kwani wakati mchujo unafanyika
sikuwepo hivyo huwezi kusema nilikuwa wamwisho wakati hata sikuwepo ndio maana
nilisema sikubali kama kweli imekuwa hivyo kwa kuwa sikuwepo ila nilijua uamuzi
ninaungoja ni wa vikao vingine na uamuzi umefanyika kwa haki na nimeridhika
bila kingongo hivyo niwajibu wangu kukisaidia chama change”alisema
Aidha kuhusu
kauli ya mwenyekiti wakewa taifa watakashindwa kupitishwa watakihama
chama hicho na kuwataka waende mapema,alisema hiyo ni kauli ya kiongozi wake
ambayo yeye hajawahi kuitoa popote wala kutoa vitisho vya namna hiyo kwa chama
chake.
No comments:
Post a Comment