Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Butiama mkoani Mara Bw Gerald Joseph
VIJANA WA CHAMA
CHA MAPINDUZI WAMEONYWA KAMWE WASIKUBALI KUTUMIWA KAMA MADARAJA YA
WATU WANAOHITAJI KUGOMBEA URAIS KUPITIA CHAMA HICHO KWA VILE KUFANYA HIVYO
KUNAWEZA KUSAMBARATISHA CHAMA HICHO NA KUPATA VIONGOZI WASIO SIFA,MAADILI HUKU
WAKIJENGA MAKUNDI YANAYOWEZA KUHATARISHA AMANI YA NCHI.
KAULI HIYO
IMETOLEWA NA MKUU WA IDARA YA UHAMASISHAJI NA CHIPUKIZI CCM TAIFA AMBAYE
PIA NI MBUNGE WA VITI MAALUM KUPITIA VIJANA MKOANI MARA MH ESTHER BULAYA
,WAKATI AKIZUNGUMZA NA VIONGOZI WA UMOJA WA VIJANA WA CHAMA CHA MAPINDUZI
KATIKA WILAYA YA BUTIAMA MKOANI MARA
HATA HIVYO
AKIZUNGUMZIA RUSHWA KATIKA CHAGUZI MBALIMBALI ZINAZOENDELEA NDANI YA CHAMA
HICHO,KIONGOZI HUYO AMEWATAKA VIJANA KUKUBALI KUTENGENEZA MAADUI WENGI KWA
KUCHUKIA RUSHWA NA KUACHA KUPOKEA AMA KUTOA RUSHWA ILI KUKIWEZESHA CHAMA HICHO
KUPATA VIONGOZI WENYE UWEZO HATA KAMA NI MASIKINI
KATIKA
KIKAO HICHO CHA VIJANA WA CCM WILAYANI BUTIAMA,MH BULAYA PIA AMEWATAKA
VIJANA KUUNDA VIKUNDI VYA UZALISHAJI VIKIWEMO VYAMA VYA KUWEKA NA KUKOPA
AMBAVYO VITAWAWEZESHA KUPATA MIKOPO KUTOKA TAASISI MBALIMBALI ZA FEDHA
IKIWA NI NJIA MOJA WAPO YA KUKABILIANA NA TATIZO KUBWA LA UKOSEFU WA
AJIRA KWA KUNDI HILO LA VIJANA.
No comments:
Post a Comment