Ukumbi wa Mikutano katika Shule ya Oswadi Mang'ombe moja ya shule iliyojengwa na Mh Mkono
Mjumbe wa kamati tendaji wa CWT wilaya ya Butiama Cyprianus Meneja akiwa ameshikilia tuzo ambayo alikabidhiwa Mh Mkono
Hati ya Heshima ya kutambua mchango wa Mh Mkono katika wilaya ya Butiama na jimbo la Musoma kwa ujumla
Mh Mkono mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini akiwa amenyanyua kinyago mfano wa Sura yake kama tuzo ya Mchnago wake kutoka Chama cha Walimu wilaya ya Butiama
Maabara ya kisasa ya Shule ya Oswald Mang'ombe iliyojengwa na Mh Mkono
Moja ya Nyumba ya kisasa inayojengwa na Mh Mkono katika jimbo la Musoma vijijini ambapo kwasasa inafahamika kama wilaya ya Butiama
Na George Marato,Butiama
KATIKA kukabiliana na tatizo kubwa la upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi unazikabili shule nyingi hapa nchini,mbunge wa jimbo la Musoma vijijini mkoani Mara Nimrod Mkono ametangaza kumjengea nyumba ya kisasa kwa kila mwalimu wa somo hilo, ambaye atakubali kufundisha somo hilo katika wilaya ya Butiama.
Akizungumza na ujembe wa Chama cha Waalimu Tanzania CWT katika wilaya ya Butiama,kabla ya chama hicho kumkabidhi hati maalum ya kutambua mchango wake katika sekta ya elimu pamoja na zawadi,mbunge huyo wa Musoma vijijini Mkono,alisema pamoja na kumjengea nyumba kila mwalimu wa somo la sayansi pia atatoa fedha kwaajili ya chama cha kuweka na kukopa kwa kila shule yenye mchepuo wa masomo ya sayansi kuanzia sasa.
Alisema lengo la hatua hiyo ni kuvutia walimu zaidi kufanya kazi katika eneo hilo la butiama hasa kwa walimu wa sayansi na ambao ni wachache katika shule za Sekondari.
Mbunge Mkono aliuaambia ujembe huo wa cwt kuwa kulingana na mabadiliko ya makubwa ya dunia ya sayansi na teknolojia hakuna budi sasa kuongeza kasi katika ufundishaji wa masomo ya sayansi katika shule za sekondari katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za dunia.
“Natangaza leo kuwa mwalimu yoyote ya soma la sayansi atakaekubali kuja kufundisha katika wilaya ya Butiama aje nimjengee nyumba nzuri na kisasa ili aweze kufanya kazi yake bila kupata tatizo la makazi”alisema Mkono na kuongeza.
“Mbali na nyumba pia nitatoa fedha za kuanzisha vyama vya kuweka na kukopa kwa kila shule ya mchepuo wa sayansi katika wilaya yangu lengo langu likiwa nikuwavutia walimu zaidi kuja katika eneo hili na kufundisha bila vikwazo vyovyote”alisema.
Kuhusu migomo ya walimu ambayo imekuwa ikijitokeza kila wakati ya kushinikiza serikali kuboresha maslahi yao,mbunge huyo wa Musoma vijijini amekishauri chama hicho kuanzia sasa kabla ya kufikia hatua hiyo kukutana nao hili kuona jinsi ya kutatua matatizo yao badala ya kugoma na kuwapa mateso makubwa wanafunzi.
“Najua walimu umekuwa na matatizo makubwa na kila leo mmekuwa na migomo migoma sasa ushauri wangu hapa kwangu kabla hamjafikia hatua hiyo mnishirikishe tuone njia sahihi ya kutatua matatizo yenu kabla ya kuwapa mateso wanafunzi wetu”aliongeza Mkono.
Akitoa salama za cwt kabla ya kukatibidhi hati hiyo maalum na zawadi maalum kama ishara ya upendo na ushirikiano,katibu wa cwt wilaya ya butiama Wanjara Nyeoja,alisema wamefikia hatua hiyo kutokana na mchango mkubwa unaotolewa na mbunge huyo katika sekta ya elimu hasa kwa kujenga shule nzuri na za kisasa zikiwemo nyumba za walimu katika jimbo hilo.
Aidha alisema bado sekta ya elimu imekuwa ikikabiliwa na changamoto lukuki zinazowakabili shule za msingi na sekondari likiwemo tatizo kubwa la ukosefu wa nyumba za walimu.
“Walimu hususani maeneo mengi ya vijijini walimu wetu wanafundisha katika mazingira magumu kwa kukosa nyumba za kuishi hata kufikia walimu wengi kufikia hatua za kuhama wilaya yetu na kusababisha upungufu mkubwa wa walimu na wanaobaki sasa wazidiwa kazi ya kufundisha watoto wetu”alisema Nyeoja.
Hata hivyo katibu huyo wa cwt,aliomba mbunge huyo kusaidia uanzishaji wa SACCOS ya walimu wa wilaya hiyo ambayo itasadia kwa kiasi kikubwa kuwapunguzia makali ya maisha yanawakabili walimu.
Kwa sababu hiyo,walimpongeza mbunge huyo kuonyesha mfano mkubwa wa kutumia raslimali zake kwaajili ya kujenga vyumba vya madarasa katika shule za msingi na sekondari zikiwemo nyumba za walimu katika jimbo hilo.
No comments:
Post a Comment