Mawasiliano muhimu popote pale
Mbunge wa Rorya Lameck Airo akifurahi pamoja na watoto wa shule ya Msingi iliyopata msaada wa madawati
Rorya
MBUNGE wa
jimbo la Rorya mkoani Mara Mh Lameck Airo,amewata ka viongozi hasa wa kisiasa kutambua
kuwa uchaguzi tayari ulikwisha hivyo ni wawajibu wao katika kuwaletea maendeleo
wananchi wao bila ya kubaguana kwa
misingi ya itikadi za kisiasa.
Mbunge huyo
wa jimbo la Rorya,ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na viongozi,wananchi na
walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Obwere katika mji mdogo wa Shirati baada
ya kukabidhi mdaa wa madawati kwa shule tatu za msingi za eneo hilo.
Amesema bado
kuna viongozi wa kisiasa wameendelea kuwa na chuki na fitina kwa kushindwa
kuwahudumia wananchi kutokana na msuguano ulitokana na uchaguzi mkuu wa mwaka
2010 jambo ambalo amesema halipaswi kupewa nafasi katika kuharakisha maendeleo
ya wananchi Rorya.
Kwa sababu
hiyo Mh Airo,amesema yeye kama mbunge amekuwa akipata vishawishi vingi kutoka
kwa baadhi ya viongozi wa chama chake cha CCM vya kumtaka kuacha kuhudimia vijiji
na kata zinazoongozwa na wapinzani vishawishi ambavyo amesema hakubaliani navyo
hata kidogo.
“Nimekuwa
nikibanwa katika vikao vyetu vya chama kwamba kwanini napeleka maendeleo maeneo
yenye viongozi wa upinzani lakini mimi nimepuuza kelele hizo kwani natambua wazi
inawezekana sisi CCM tulifanya makosa kuwapelekea mgombea ambaye hawakumtaka
sasa iweje leo tuwaadhibu”alisema na kuongeza.
“Umefika
wakati tusahau tofauti zitu zote na kuacha itikadi za vyama vyetu katika
kuwahudumia wananchi na tukifanya hivyo kwa kila kiongozi kwa mshikamano
ninaamini Rorya itapata maendeleo makubwa kwa kipindi kifupi tu”alisema Airo.
Kwa sababu
hiyo amewataka viongozi wote katika jimbo hilo kuiga mfano wake na kuacha
kuhudumia wananchi kwa misingi ya itikadi jambo ambalo linaweza kusababisha
ubaguzi mkubwa ukiwemo wa koo na koo.
Mbunge
Airo,alisema hivi sasa kwa kutumia fedha za mfuko wa jimbo atahakikisha
anapeleka katika shule zote za sekondari huduma ya maji safi na salama ili
kuondolea adha wanafunzi ambao wamekuwa wakikatisha masomo kwa kufuata maji.
Naye diwani
wa kata Mkoma Godwin Lazaro(Chadema)amempongeza mbunge huyo kwa jinsi
anavyotumia kipato chake kwahudumia wananchi kwa kila sekta bila ya ubaguzi.
Alisema
ingawa mbunge huyo anatokana na CCM lakini amekuwa na ushirikiano mkubwa na
viongozi wote katika jimbo hilo jambo ambalo limefanya wilaya hiyo kuwa na
mshikamano mkubwa ukiacha viongozi wachache wanashindwa kutambua mfumo wa kuwepo
kwa vyama vingi nchini.
“Kwa niaba
ya wananchi wa Mkoma,kwa kweli mbunge tunakuombea maisha marefu ingawa chama
chako cha CCM tukikiombea maisha mafupi ila tunapaswa kuiga mfano mnzuri ambao wa
mshikamano unatoonyesha sisi viongizi na
tukifanya hivyo kila mmoja nina uhakika hali ya leo ya maendeleo haiwezi kuwa
sawa na kesho”alisema diwani huyo.
Hata hivyo diwani
huyo wa Mkoma,alisema ni wajibu wananchi kuchangia maendeleo hasa ya sekta ya
elimu katika maeneo yao na kwamba endapo hawataki kufanya hivyo wanapaswa
kuacha kuzaa ikiwa ni njia moja wapo ya kuondokana na kero ya michango.
Kabla ya
kupokea msaada wa madawati hayo,mwalimu mkuu wa shule ya Obwere Chiliko
Magati,alisema shule hiyo pekee inakabiliwa na upungufu wa madawati 187 jambo
ambalo limefanya idadi kubwa ya wananzi kusoma wakiwa wamekaa chini.
Mbali na
shule ya Obwere kupewa msaada huo wa madawati shule nyingine ambazo zimenufaika
na msaada huo ni pamoja na Kiariko na Ngasaro zote ziko katika eneo la Shirati.
No comments:
Post a Comment