Friday, August 31, 2012

WEWE NANI KAMA MTOTO MAGRETH COSMAS ?

Bi Magreth Cosmas,mtangazaji maarufu nchini akiwa ndani ya Studio za Radio One Stereo akifanya vitu vyake......
Shemeji wa George Marato wakiwa katika nyuso za furaha....

Thursday, August 30, 2012

MATUKIO MBALIMBALI YA MBIO ZA MWENGE NYUMBANI KWA MWALIMU NYERERE WILAYA YA BUTIAMA

 Baadhi ya askari wa jeshi la polisi mkoa wa Mara wakiwa nje ya lango la Nyumba ya Baba wa taifa hayati Mwl Julius Nyerere wakingojea Mwenge wa uhuru ukiwa umechukuliwa kwenda kuwasha Mwenge wa Mwingo hivi karibuni.
 Kiongozi w mbio za Mwenge kitaifa mwaka 2012 kapt Honest Ernest Mwanossa akitamka manane Sisi tumekwisha uwasha Mwenge na kuuweka mlima Kilimanjaro,baada ya kuwasha Mwenge uliopo Mwitongo Nyumbani kwa Baba wa taifa hayati Mwl Julius K Nyerere.
 Mbunge wa Musoma vijijini Mh Nimrod Mkono,akiongoza wakimbiza mwenge wa uhuru wakati wa kuwasha Mwenge wa Mwitongo
 Kapt Honest Mwanossa,kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa mwaka 2012 akishuka baada ya kutekeleza wajibu wake wa kuwasha Mwenge wa Mwitongo ambapo kila mwaka Mwenge wa Uhuru lazima upite katika eneo hilo na kuwasha Mwenge huo Nyumbani kwa Baba wa taifa Hayati Mwl Julius Nyerere kijijini Butiama
 Wakimbiza Mwenge kitaifa na baadhi ya makamanda wa jeshi la polisi wakishuka baada ya kuwasha mwenge wa Mwitongo
Wakimbiza mwenge wa uhuru kitaifa,wakiongozwa na mkimbiza mwenge kitaifa mwaka 2012 Kapt Honest Ernest Mwanossa wakiweka mshada ya maua katika kaburi la Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere eneo la Mwitongo kijijini Butiama mkoani Mara hivi karibuni,baada ya Mwenge wa uhuru kuzuru nyumbani kwa Mwasisi wa Mwenge huo na taifa la Tanzania.

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA BLOG YA GEORGE MARATO



Mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Mh NIMROD MKONO akicheza ya Ritungu ambayo inachezwa na makabila ya Wakurya,Wazanaki,Wasimbiti,Wakiroba na jamii nyingine ya mkoa wa Mara hasa katika sherehe mbalimbali za heshima,hapa wananchi wa kijiji cha Mwibagi wakimpongeza mbunge huyo baada ya kujenga barabara kwaajili ya kurahisisha mawasiliano

Mwandishi mwandamizi wa ITV na Radio One George Marato akiwa nje ya ukumbi wa Bunge hivi karibuni mjini Dodoma
Mwandishi mwandamizi wa ITV na Radio One George Marato akiwa nje ya ukumbi wa Bunge hivi karibuni mjini Dodoma
Mhariri wa habari wa ITV na Radio One Stephen Chuwa mwenye vazi maalum linalovaliwa na watu wa nchi za Magharibi akiwa na mwandishi mwandamizi wa ITV na Radio One katika sherehe iliyoandalwa na mwenyekiti wa makampuni ya IPP Dk Reginald Mengi kwaajili ya kujipongeza baada ya kumaliza mwaka 2011 katika ukumbi maarufu wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari wa ITV na Radio One wakiwa katika sherehe iliyoandaliwa na mwenyekiti wa IPP Dr Reginald Mengi,mwenye tai ni mwandishi mwandamizi George Marato mkoani Mara
Hawa ni baadhi ya maafisa wa JWTZ katika kikosi cha Makoko Musoma wakiwa katika maandalizi ya sherehe za kutimiza miaka 48 ya kuanzishwa kwa JWTZ
Kila kazi inaugumu wake huyu ni askari wa JWTZ akitoa heshima kwa Amiri jeshi mkuu Rais Jakaya Kikwete hayupo pichani wakati wa mazishi ya mkuu wa majeshi mstaafu Generali Mwita Kyaro
Hii ni moja ya barabara zinazojengwa na mbunge wa Musoma vijijini Mh NIMROD MKONO,katika kufungua mawasiliano katika jimbo lake.
Serikali ina kila sababu kuwaeleza wananchi mgodi wa Buhemba ni mali ya nani,haya ni mabaki ya mgodi huo ambao ulisababisha hasara ya zaidi ya bilioni 30 kwa wananchi wanazunguka mgodi huo
Wilaya ya Bunda imeanza kutekeleza mradi wa kuwapatia wananchi hati miliki za ardhi wananchi wake ili kuwawezesha kutumia hati hizo kukopa katika vyombo vya fedha kama njia moja wapo ya kujikomboa na umasikini
Diwani wa kata ya Buhemba,akizungumzia madhara yaliyosababishwa na uwekezaji wa mgodi wa Buhemba,hivi sasa wananchi hao wanadai zaidi ya bilioni 30 kama fidia iliyosababishwa na mgodi huo uliodaiwa ni wa jeshi kupitia kampuni ya Meremeta

HATA WANAWAKE WAMO WAKIWEZESHWA

Mmoja ya wafanyakazi wa ITV kitengo cha kuchanganya picha akifanya vitu vyake...yeye si tu amebobea katika kuchanganya picha hata kushika camera yumo

Mbunge wa Musoma vijijini Nimrod Mkono akiwa pamoja na mwandishi wa ITV na Radio One katika moja ya vikao.

Mwandishi wa habari wa ITV/Radio One mkoani Mara George Marato akishauriana jambo na mbunge wa Musoma vijijini kabla ya kuanza kwa kikao cha ushauri cha mkoa RCC mkoani Mara.

Mwandishi wa ITV na Radio One mkoa wa Mara na mzee Yusuf Makamba

Alikuwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam mzee Yusuf Rajab Makamba akizungumza na ITV baada ya kuongoza harambee ya kuchangia mfuko wa elimu mkoani Mara

JENGO LENYE KABURI LA BABA WA TAIFA ENEO LA MWITONGO BUTIAMA

Makamu wa CCM Tanzania Bara mzee Pius Msekwa mwenye shati la kijani katika akiwa na mwenyekiti wa ccm mkoa Mara Bw Cherles Makongoro Nyerere na viongozi wengine wa kijiji cha Butiama wakitoka ndani ya banda lilimo kaburi la Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius K Nyerere,kutoa heshima wakati mzee msekwa alipotembelea familia ya baba wa taifa kijiji hapo.

 
Na George Marato,Musoma

VITA ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015,imetajwa kuwa chanzo cha kuhakikisha lazima Makongoro Nyerere ang’olewe katika kutetea nafasi yake uenyekiti wa CCM mkoa wa Mara kwenye uchaguzi unaotarajia kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Makongoro ambaye ni mtoto wa tano wa Baba wa taifa hayati mwalimu Julius Nyerere,amekuwa mwenyekiti wa ccm mkoa wa Mara kwa miaka mitano inayomalizika sasa,amethibitisha kuwapo kwa njama hizo ambazo amedai zinatokana na msimamo wake wa kutaka chama kuwafukuza viongozi ambao kwa namna moja ama nyingine wamekuwa wakituhumiwa kwa ufisadi na kusababisha kushusha heshima ya chama hicho mbele ya jamii.

Alisema kutokana na msimamo huo, kuna baadhi ya watu wanaominika kumuunga mkono mmoja ya watu wanaotajwa kugombea nafasi ya urais mwaka 2015 kupitia chama hicho na wenye uwezo mkubwa kifedha wakiwa nje na ndani ccm mkoani Mara,wamepanga kununua kila kura ya mjumbe mmoja wa mkutano mkuu kwa shilingi laki moja hadi laki moja na nusu ili kuhakikisha mwanasiasa huyo anang’oka katika nafasi hiyo.

“Ni kweli nimepata taarifa kuna fungu kubwa limepangwa ili kuhakikisha linaning’oa ndio maana wamemfuta mmoja ya watu ambao historia inaonyesha miaka yote walikuwa hawaivi lakini sasa wamemshawishi kuchukua fomu na kumchangia fedha ili kufanikisha mkakati wao…lakini mimi sina wasiwasi hata kidogo nimechukua fomu naijaza na kurejesha kwani najua wenye uamuzi wa mwisho ni wajumbe wa mkutano mkuu sio fedha zao”alisema Makongoro kwa njia ya simu endapo anatetea nafasi yake hiyo.


Inadaiwa kuwa chuki kubwa za kuhakikisha Makongoro anang’olewa katika nafasi hiyo hata bila kujali gharama zitakazotumika nikutokana na msimamo wake katika kukiongoza chama hicho bila kuhitaji kundi pili kukataa kwake kupanda majukwaani mwaka 2010 katika uchaguzi mkuu ili aweze kumtukana mdogo wake Vicent Nyerere aliyekuwa anagombea ubunge kupitia Chadema.

Kwa mujibu wa habari kutoka ndani ya ccm Musoma mjini na kutoka kwa baadhi ya viongozi wa mkoa,walimshinikiza Makongoro kutumia ukaribu wake na mgombea huyo wa Chadema kupanda katika majukwaa na kumshambulia hata kumkana kuwa si ndugu yake kama mkakati ambao ungesaidia ccm kushinda katika jimbo la Musoma mjini, jambo ambalo lilipingwa vikali na Makongoro kwa madai hawezi kumtolea lugha ya matusi mdogo wake kwa misingi tu ya siasa.


Kutokana na msimamo huo wa Makongoro ulimfanya kuchukiwa na baadhi ya viongozi wa ccm wa mkoa tena wenye ushawishi mkubwa kifedha na wale wa Musoma mjini hivyo kuanza mikakati mbalimbali ya kumng’oa kupitia katika vikao lakini walishindwa,pia wakajitokeza kumchafua wakati akigombea ubunge wa afrika mashariki mkakati ambao pia ulishindwa na hivi sasa nguvu kubwa imeelekezwa katika uchaguzi huo.

Hadi jana tayari wanachama watatu wa ccm,wamechukua fomu za kugombea nafasi ya uenyekiti wa ccm mkoa wa Mara pamoja na Makongoro,pia wamo Dommy Athumani Juma na aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho miaka kumi iliyopita Enock Mwita Chambiri kabla ya kutangaza kustafu nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu wa chama hicho mwaka 2007.

Chambiri alitangaza kustafu uenyekiti mwaka 2007 katika mkutano mkuu wa uchaguzi wa chama hicho,ambao ulimwingiza Makongoro madarakani kwa kusoma alama za nyakati wakati huo kutokana na makundi yalikuwepo na kumpinga huku akisema anaiachia nafasi hiyo lakini atasita kurudi tena endapo ataona chama hicho kinayumba.

Vita ya Makongoro pia imeelezwa inaweza kumkumba mbunge wa Musoma vijijini Nimrod Mkono ambaye tayari amechukua fomu za kugombea uenyekiti wa wazazi taifa baada ya kutuhumiwa kuwa ndiye aliyemsadia Makongoro Nyerere kushinda vita ubunge wa afrika mashariki.

Wakati huo huo kasi ya wanachama wa CCM kuchukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali
za uongozi ndani ya chama hicho mkoani Mara inazidi kuongezeka hasa katika nafasi za ujumbe wa halmashauri kuu kupitia wilaya.

Miongoni mwa vigogo walichukua fomu hizo ni mfanyabiashara maarufu Christopher Gachuma(Tarime),Thobias Raya(Rorya) Marwa Siagi(Musoma vijijini),Vedastus Mathayo (Musoma mjini) akiwemo mwandishi mwandamizi wa habari Cyprian Musiba
kujitosa kuomba nafasi hiyo katika wilaya ya Bunda.

Mchuano katika nafasi za halmashauri kuu taifa kupitia ngazi ya wilaya unatarajia kuwa mkali zaidi kutokana na idadi kubwa ya wanachama kujitokeza kuchukua fomu hizo.