Friday, October 12, 2012

MRADI MKUBWA WA MAJI MAJI KUANZA KUTEKELEZWA MUSOMA MJINI


-Pia watumishi wa idara ya maji Mugango,Kiabakari na Butiama wafikisha madai ya mishahara ya miezi 26 hadi miaka mitatu

-Pia hakuna mwandishi aliyeshushwa na Muwasa kushiriki katika ziara ya naibu waziri kama ilivyoripotiwa awali

HATIMAYE Serikali imepanga kutekeleza mradi mkubwa wa maji katika Manispaa ya Musoma mkoani Mara ambao unatarajia kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 41.

Naibu waziri wa Maji Mh Mhandisi Dk Benilith Mahenge,ametoa taarifa hiyo mjini Musoma wakati akizungumza na uongozi wa mkoa wa Mara,ambapo amesema tayari mipango wa kuanza utekelezaji wa mradi huo mkubwa imekamilika baada ya serikali kupata fedha kutoka nchi za Ujerumani na Ufaransa.
Amesema mradi huo pamoja na kuchelewa kuanza utekelezaji wake kwa zaidi ya miaka mitatu lakini utalenga kuhamisha chanzo cha maji cha sasa na kujengwa upya katika eneo la Bukanga pamoja na kufufua na kuongeza miundombinu  mipya ya maji ili kukidhi hitaji  la maji kwa wananchi na taasisi zote katika Manispaa ya Musoma.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Mara Bw John Tupa,pamoja na kupongeza hatua hiyo ya serikali kwa kukubali kutekeleza mradi huo katika unaolenga kuwandolea kero kubwa ya upungufu wa maji inayowakabili wananchi lakini pia ameahidi kuwa serikali ya mkoa itahakikisha inapambana na vitendo vyote vya hujuma ambayo inaweza kujitokeza katika utekelezaji wa mradi huo.

Wakati huo huo baadhi ya watumishi wa serikali katika mradi wa maji wa Mugango,Kiabakari hadi Butiama wanadai mishahara yao ya kati ya miezi 26 hadi 30 jambo ambalo limewafanya kuishi maisha ya kuomba omba.

Wafanyakazi hao wametoa kilio hicho baada ya naibu waziri wa Maji Mh Mhandisi Dk Binilith Mahenge kutembelea mradi huo ambao pia umekuwa ukikabiliwa na uchakavu mkubwa wa miundombinu ya kusambazia maji kenda kwa wananchi ikiwemo familia ya baba wa Taifa hayati Mwl Julius Nyerere.

Wakiwa na mabango wafanyakazi hao ambao wengi ni vibarua wa kudumu wamemueleza na naibu waziri huyo kwa nyakati tofauti kuwa  hivi sasa baada ya kutoka kazini wanalazimika kufanya vibarua vikiwemo vya kulima mashamba kwaajili ya kupata fedha za kuhudumia familia zao.

Kufuatia kilio hicho,naibu waziri huyo wa maji,ameuagiza uongozi wa mamlaka ya maji ya Mugango,Kibakari hadi Butiama,halmashauri ya Musoma na ofisi ya mkuu wa wilaya ya Butiama kumpatia maelezo ya sababu za wafanyakazi hao kutolipwa mishahara yao kwa kipindi hicho pamoja na kuorodhesha madai yote ambayo yanadaiwa na watumishi hao ndani ya siku tatu.

Amesema kushindwa kulipa mishahara hiyo kwa wakati kunaweza kuchangia watumishi wasio waaminifu kufanya hujuma kubwa ikiwa ni pamoja na kuiba mashine za mradi huo jambo ambalo linaweza kuingizia hasara kubwa serikali huku  akitoa mwezi mmoja kwa meneja wa mradi huo mhandisi Merchedes Tibita kuongeza ukusanyaji wa mapato ambayo yatawezesha kutatua baadhi ya changamoto zinazoukabili mradi huo.

ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA MAJI MH ENG DK BINILITH MAHENGE WILAYA ZA MUSOMA NA BUTIAMA




Naibu waziri wa Maji Mh Dk Binilith Mahenge akiwa pamoja na DC Musoma Jackison Msome na mkurugenzi wa MUWASA Gines Kaduei
 Mh Mahenge akiwa pamoja na viongozi wa wilaya ya Butiama
 Meya wa Manispaa ya Musoma Alex Kisurura wa kwanza kulia akiwa na naibu waziri wa maji na viongozi wa Manispaa ya Musoma
 Picha ya juu mkurugenzi wa Muwasa akimunyesha mitambo naibu waziri wa maji
 Chanzo cha maji cha Muwasa katika ziwa victoria ambacho kinahitajika kuhamishwa kwa gharama ya bilioni 41 kwaajili ya kuwezesha mji wa Musoma kupata maji ya uhakika
 Sehemu ya mji wa Butiama
 Viongozi wa wilaya ya Butiama wakiwa na naibu waziri wa maji wa kwanza kushoto ni Magina Magesa m/kiti wa halmashauri ya Musoma
 Chanzo cha maji cha mradi wa Mugango,Kiabakari hadi Butiama
 Naibu waziri akiwa pamoja viongozi wa wilaya ya Butiama
 Bango la wafanyakazi wa maji Mugango/Butiama ambao wanaidai serikali miezi 26 hadi miaka mitatu
 Sehemu ya mji wa Butiama

 Naibu waziri wa maji Mh Mahenge akisoma moja ya bango
 Naibu waziri wa maji akiangalia Bwawa la Kiarano


 Naibu waziri akitoa heshima katika kaburi la Baba wa taifa kijijini Butiama

 Emanuel Ams wa TBC akisalimiana na mjane wa baba wa Taifa mama Maria Nyerere
 Naibu waziri akisalimiana na mama Maria Nyerere
 Naibu waziri akitoa neno la shukurani kwa Mama Maria Nyerere


Monday, October 8, 2012

PICHA NA MATUKIO KATIKA ZIARA YA MANAIBU MAWAZIRI Mh Masele Na Kitwanga katika mgodi wa North Mara wilayani Tarime

 Naibu waziri ofisi ya Makamu wa Rais Mh Chaerles Kitwanga akizungumza na waandishi baada kumaliza ziara yao katika mgodi wa North Mara unaomilikiwa na ABG
 Picha ya juu ni picha ya pamoja ya manaibu waziri wa Madini na Mazingira ofisi ya makamu wa rais Stephen Masele na Charles Kitwanga pamoja na makamu wa Rais wa ABG Tanzania Deo Mwanyika na mkuu wa wilaya ya Tarime na chini yake na wajenzi wakiendelea na kazi katika shule ya Sekondari ya Ingwe inayojengwa na ABG
 Moja ya jengo yanayokarabatiwa na ABG zinazozunguka mgodi wa North Mara
 Manaibu waziri wakitembezwa kukagua ukarabati wa majengo ya shule
 Kazi ya ukarabati ukiendelea kwa kasi

 Moja ya viwanja vinavyoandaliwa kwa ujenzi wa shule za msingi Matongo na Nyamongo ambazo zinahamishwa toka maeneo ya awali ili kuepukana na vumbi linalosababishwa na uchimbaji wa dhahabu,ujenzi ambao utagharimu ABG dola milioni 3

 Pamoja na kuwachimbia visima vya maji pia ABG kupitia mgodi wake wa North Mara unawasambazia maji safi na salama wananchi katika maeneo yao
 Waandishi wakiwa kazini
 Manaibu waziri wa Nishati Mh Stephen Masele na wa Mazingira Charles Kitwanga wakifungua moja ya visima vya maji
 Waandishi kazini
 Manaibu waziri wakiwa na viongozi wa mgodi na mkuu wa wilaya ya Tarime John Henjewele
 Makamu wa rais kulia akiwanyesha kitu mawaziri
 Ufunguzi wa kisima katika kijiji cha Nyamwaga
 M/kiti wa kijiji Nyamwaga Bw Sasi akiipongeza ABG kwa kuwachimbia kisima

 Naibu waziri Charles Kitwanga akimtwisha maji mama mmoja baada ya kisimu kuzinguliwa
 Naibu waziri Stephen Masele katika picha ya pamoja na watumizi wa kituo cha afya cha Sungusungu kilichokarabatiwa na mgodi wa North Mara
 Mmoja ya watu wanakatana mapanga wenyewe kwa wenyewe kwa kugombania mawe ya mgodi
 Deo Mwanyika akijiandaa kujibu maswali ya waandishi wa habari
 Mh Masele akiwa na baadhi ya viongozi wa mgodi
 Picha ya pamoja manaibu waziri na uongozi wa ABG na Serikali




 Zahanati ya Sungusungu iliyokarabatiwa na ABG
 Sehemu ya polisi walikuwa katika ziara ya viongozi hao



 Mashine inayotumika kufyatua matofari ya kujengea shule mpya ambazo zinahamishwa kupisha uchimbaji wa dhahabu

 Mh Masele akisisitiza jambo
 Sehemu ya matofari yanayotarajia kutumika kujenga shule mbili mpya

 Mh Kitwanga akizungumza baada ya ziara yake North Mara
 Mh Masele akizungumza na waandishi
 Sehemu ya mgodi wa North Mara


 Sehemu ya wafanyakazi wa North Mara wakijiandaa kuzungumza na naibu waziri Nishati


 Meneja wa mgodi wa North Mara Bw Gray Chapman akitoa maelezo kabla ya naibu waziri Nishati kuzungumza na wafanyakazi

 Mh Masele akizungumza na wafanyakazi
 Moja ya shimo linalichimbwa katika eneo la Gokona North Mara
Viongozi wakitazama shughuli za uchimbaji