Wednesday, September 26, 2012

MAONI YA MH NIMROD MKONO KUHUSU UTEUZI WA WAGOMBEA NDANI YA CHAMA HICHO.


Mmmoja ya watu walijitokeza kugombea uenyekiti kupitia jumuiya ya wazazi wa chama cha mapinduzi taifa Nimrod Mkono,amesema anaunga mkono kwa asilimia mia moja maamzi yote ya vikao vya uteuzi wa wagombea.
Alisema kuteuliwa yeye hakuna maana kuwa kuna jambo limekosewa bali ni taratibu za chama na kwamba kwa asilimia mia moja anaunga mkono uamuzi huo ambao umefanywa katika vikao mbalimbali vikiwemo vile vilivyokuwa chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete jana.
“Mimi ni mwana ccm damu ninaunga mkono uamuzi wa chama changu tena kwa asimia mia moja,walioteuliwa ni wanaccm wenzangu ninatoa ahadi ya kuwapa ushirikiano wa kutosha hadi tutakapo pata mmoja wetu kuwa kiongozi wa jumuiya yetu”alisema Mkono.
Kuhusu kauli yake kuwa endapo hatapitishwa jina lake hapatatosha ndani ya CCM alisema kauli ile aliitoa kwa kusema kuwa hakubaliani nay ale yaliandikwa kwenye magazeti kwa vile kulikuwa bado kuna vikao vilikuwa vikiendelea ndani chama hicho.
“Nilisema sikubaliani nay ale yaliandikwa kwenye magazeti kwani wakati mchujo unafanyika sikuwepo hivyo huwezi kusema nilikuwa wamwisho wakati hata sikuwepo ndio maana nilisema sikubali kama kweli imekuwa hivyo kwa kuwa sikuwepo ila nilijua uamuzi ninaungoja ni wa vikao vingine na uamuzi umefanyika kwa haki na nimeridhika bila kingongo hivyo niwajibu wangu kukisaidia chama change”alisema
Aidha kuhusu kauli ya mwenyekiti wakewa taifa  watakashindwa kupitishwa watakihama chama hicho na kuwataka waende mapema,alisema hiyo ni kauli ya kiongozi wake ambayo yeye hajawahi kuitoa popote wala kutoa vitisho vya namna hiyo kwa chama chake.

VIJANA WAASWA KUTOKUWA DARAJA KWA WATU KUFANIKISHA MALENGO YAO


 Vifaa vilivyogawa kwaq kata 34 za wilaya ya Butiama mkoani Mara leo na Mh Esther Bulaya
 Mh Esther Bulaya akitoa neno kwa vijana wa kata 34 kutoka wilaya ya butiama mkoani Mara
 Katibu wa CCM wilaya ya Butiama mkoani Mara Bi Mercy Maramboakiwaasa Vijana wa CCM kutoka wilaya hiyo
 Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Butiama mkoani Mara Bw Gerald Joseph
 Picha ya Pamoja na Viongozi wa kata 34 za wilaya ya Butiama mkoani Mara wakiwa na nyuso za Furaha baada ya kukabidhiwa Vifaa hivyo



VIJANA WA CHAMA CHA MAPINDUZI WAMEONYWA KAMWE WASIKUBALI  KUTUMIWA KAMA MADARAJA  YA WATU WANAOHITAJI KUGOMBEA URAIS KUPITIA CHAMA HICHO KWA VILE KUFANYA HIVYO KUNAWEZA KUSAMBARATISHA CHAMA HICHO NA KUPATA VIONGOZI WASIO SIFA,MAADILI HUKU WAKIJENGA MAKUNDI YANAYOWEZA KUHATARISHA AMANI  YA NCHI. 

KAULI HIYO IMETOLEWA NA MKUU WA  IDARA YA UHAMASISHAJI NA CHIPUKIZI CCM TAIFA AMBAYE PIA NI MBUNGE WA VITI MAALUM KUPITIA VIJANA MKOANI MARA MH ESTHER BULAYA ,WAKATI AKIZUNGUMZA NA VIONGOZI WA UMOJA WA VIJANA WA CHAMA CHA MAPINDUZI KATIKA WILAYA YA BUTIAMA MKOANI MARA

HATA HIVYO AKIZUNGUMZIA RUSHWA KATIKA CHAGUZI MBALIMBALI ZINAZOENDELEA NDANI YA CHAMA HICHO,KIONGOZI HUYO AMEWATAKA VIJANA KUKUBALI KUTENGENEZA MAADUI WENGI KWA KUCHUKIA RUSHWA NA KUACHA KUPOKEA AMA KUTOA RUSHWA ILI KUKIWEZESHA CHAMA HICHO KUPATA VIONGOZI WENYE UWEZO HATA KAMA NI MASIKINI

 KATIKA KIKAO HICHO CHA  VIJANA WA CCM WILAYANI BUTIAMA,MH BULAYA PIA AMEWATAKA VIJANA KUUNDA VIKUNDI VYA UZALISHAJI VIKIWEMO VYAMA VYA KUWEKA NA KUKOPA AMBAVYO VITAWAWEZESHA KUPATA MIKOPO KUTOKA TAASISI MBALIMBALI  ZA FEDHA IKIWA NI NJIA MOJA WAPO YA KUKABILIANA NA TATIZO KUBWA LA UKOSEFU  WA AJIRA KWA KUNDI HILO  LA VIJANA.

Tuesday, September 25, 2012

Muda wa siasa ulikwisha mwaka 2010 sasa ni muda wa kuwahudumia wananchi bila ya itikadi-Airo

         Mbunge wa Rorya Lameck Airo kushoto akiwa katika moja ya darasa  jimbo kwake
             Mawasiliano muhimu popote pale
 Mbunge wa Rorya Lameck Airo akifurahi pamoja na watoto wa shule ya Msingi iliyopata msaada wa madawati

Rorya

MBUNGE wa jimbo la Rorya mkoani Mara Mh Lameck Airo,amewata ka viongozi hasa wa kisiasa kutambua kuwa uchaguzi tayari ulikwisha hivyo ni wawajibu wao katika kuwaletea maendeleo  wananchi wao bila ya kubaguana kwa misingi ya itikadi za kisiasa.

Mbunge huyo wa jimbo la Rorya,ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na viongozi,wananchi na walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Obwere katika mji mdogo wa Shirati baada ya kukabidhi mdaa wa madawati kwa shule tatu za msingi za eneo hilo.

Amesema bado kuna viongozi wa kisiasa wameendelea kuwa na chuki na fitina kwa kushindwa kuwahudumia wananchi kutokana na msuguano ulitokana na uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 jambo ambalo amesema halipaswi kupewa nafasi katika kuharakisha maendeleo ya wananchi Rorya.

Kwa sababu hiyo Mh Airo,amesema yeye kama mbunge amekuwa akipata vishawishi vingi kutoka kwa baadhi ya viongozi wa chama chake cha CCM vya kumtaka kuacha kuhudimia vijiji na kata zinazoongozwa na wapinzani vishawishi ambavyo amesema hakubaliani navyo hata kidogo.

“Nimekuwa nikibanwa katika vikao vyetu vya chama kwamba kwanini napeleka maendeleo maeneo yenye viongozi wa upinzani lakini mimi nimepuuza kelele hizo kwani natambua wazi inawezekana sisi CCM tulifanya makosa kuwapelekea mgombea ambaye hawakumtaka sasa iweje leo tuwaadhibu”alisema na kuongeza.

“Umefika wakati tusahau tofauti zitu zote na kuacha itikadi za vyama vyetu katika kuwahudumia wananchi na tukifanya hivyo kwa kila kiongozi kwa mshikamano ninaamini Rorya itapata maendeleo makubwa kwa kipindi kifupi tu”alisema Airo.

Kwa sababu hiyo amewataka viongozi wote katika jimbo hilo kuiga mfano wake na kuacha kuhudumia wananchi kwa misingi ya itikadi jambo ambalo linaweza kusababisha ubaguzi mkubwa ukiwemo wa koo na koo.

Mbunge Airo,alisema hivi sasa kwa kutumia fedha za mfuko wa jimbo atahakikisha anapeleka katika shule zote za sekondari huduma ya maji safi na salama ili kuondolea adha wanafunzi ambao wamekuwa wakikatisha masomo kwa kufuata maji.

Naye diwani wa kata Mkoma Godwin Lazaro(Chadema)amempongeza mbunge huyo kwa jinsi anavyotumia kipato chake kwahudumia wananchi kwa kila sekta bila ya ubaguzi.

Alisema ingawa mbunge huyo anatokana na CCM lakini amekuwa na ushirikiano mkubwa na viongozi wote katika jimbo hilo jambo ambalo limefanya wilaya hiyo kuwa na mshikamano mkubwa ukiacha viongozi wachache wanashindwa kutambua mfumo wa kuwepo kwa vyama vingi nchini.

“Kwa niaba ya wananchi wa Mkoma,kwa kweli mbunge tunakuombea maisha marefu ingawa chama chako cha CCM tukikiombea maisha mafupi ila tunapaswa kuiga mfano mnzuri ambao wa mshikamano unatoonyesha sisi viongizi  na tukifanya hivyo kila mmoja nina uhakika hali ya leo ya maendeleo haiwezi kuwa sawa na kesho”alisema diwani huyo.

Hata hivyo diwani huyo wa Mkoma,alisema ni wajibu wananchi kuchangia maendeleo hasa ya sekta ya elimu katika maeneo yao na kwamba endapo hawataki kufanya hivyo wanapaswa kuacha kuzaa ikiwa ni njia moja wapo ya kuondokana na kero ya michango.

Kabla ya kupokea msaada wa madawati hayo,mwalimu mkuu wa shule ya Obwere Chiliko Magati,alisema shule hiyo pekee inakabiliwa na upungufu wa madawati 187 jambo ambalo limefanya idadi kubwa ya wananzi kusoma wakiwa wamekaa chini.

Mbali na shule ya Obwere kupewa msaada huo wa madawati shule nyingine ambazo zimenufaika na msaada huo ni pamoja na Kiariko na Ngasaro zote ziko katika eneo la Shirati.

Wednesday, September 19, 2012

MH MKONO APEWA TUZO YA HESHIMA NA CHAMA CHA WALIMU WILAYA YA BUTIAMA

     Hati ya Pongezi Maalum ya kutambua mchango wa Mh Nimrod Mkono katika sekta ya Elimu jimbo la Musoma vijijini kwasasa wilaya ya Butiama

  Ukumbi wa Mikutano katika  Shule ya Oswadi Mang'ombe moja ya shule iliyojengwa na Mh Mkono
   Mjumbe wa kamati tendaji wa CWT wilaya ya Butiama Cyprianus Meneja akiwa ameshikilia tuzo ambayo alikabidhiwa Mh Mkono
 Hati ya Heshima ya kutambua mchango wa Mh Mkono katika wilaya ya Butiama na jimbo la Musoma kwa ujumla
   Mh Mkono mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini akiwa amenyanyua kinyago mfano wa Sura yake kama tuzo ya Mchnago wake kutoka Chama cha Walimu wilaya ya Butiama
                   Maabara ya kisasa ya Shule ya  Oswald Mang'ombe iliyojengwa na Mh Mkono

Moja ya Nyumba ya kisasa inayojengwa na Mh Mkono katika jimbo la Musoma vijijini ambapo kwasasa inafahamika kama wilaya ya Butiama

Na George Marato,Butiama

KATIKA kukabiliana na tatizo kubwa la upungufu  wa walimu wa masomo ya sayansi unazikabili shule nyingi hapa nchini,mbunge wa jimbo la Musoma vijijini mkoani Mara Nimrod Mkono ametangaza kumjengea nyumba ya kisasa kwa kila mwalimu wa somo hilo, ambaye atakubali kufundisha somo hilo katika wilaya ya Butiama.

Akizungumza na ujembe wa Chama cha Waalimu Tanzania CWT katika wilaya ya Butiama,kabla ya chama hicho kumkabidhi  hati maalum ya kutambua  mchango wake katika sekta ya elimu pamoja na zawadi,mbunge huyo wa Musoma vijijini  Mkono,alisema pamoja na kumjengea nyumba  kila mwalimu wa somo la sayansi pia atatoa fedha kwaajili ya chama cha kuweka na kukopa kwa kila shule yenye mchepuo wa masomo ya sayansi kuanzia sasa.

Alisema lengo la hatua hiyo ni kuvutia walimu zaidi kufanya kazi katika eneo hilo la butiama hasa kwa walimu wa sayansi na ambao ni wachache katika shule za Sekondari.

Mbunge Mkono aliuaambia ujembe huo wa cwt kuwa kulingana na mabadiliko ya makubwa ya dunia ya sayansi na teknolojia hakuna budi sasa kuongeza kasi katika ufundishaji wa masomo ya sayansi katika shule za sekondari katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za dunia.

“Natangaza leo kuwa mwalimu yoyote ya soma la sayansi atakaekubali kuja kufundisha katika wilaya ya Butiama aje nimjengee nyumba nzuri na kisasa ili aweze kufanya kazi yake bila kupata tatizo la makazi”alisema Mkono na kuongeza.

“Mbali na nyumba pia nitatoa fedha za kuanzisha vyama vya kuweka na kukopa kwa kila shule ya mchepuo wa sayansi katika wilaya yangu lengo langu likiwa nikuwavutia walimu zaidi kuja katika eneo hili na kufundisha bila vikwazo vyovyote”alisema.

Kuhusu migomo ya walimu ambayo imekuwa ikijitokeza kila wakati  ya kushinikiza serikali kuboresha maslahi yao,mbunge huyo wa Musoma  vijijini amekishauri chama hicho kuanzia sasa kabla ya kufikia hatua hiyo kukutana nao hili kuona jinsi ya kutatua matatizo yao badala ya kugoma na kuwapa mateso makubwa wanafunzi.

“Najua walimu umekuwa  na matatizo makubwa na kila leo mmekuwa na migomo migoma sasa ushauri wangu hapa kwangu kabla hamjafikia hatua hiyo mnishirikishe tuone njia sahihi ya kutatua matatizo yenu kabla ya kuwapa mateso wanafunzi wetu”aliongeza Mkono.

Akitoa salama za cwt kabla ya kukatibidhi hati hiyo maalum na zawadi maalum kama ishara ya upendo na ushirikiano,katibu wa cwt wilaya ya butiama Wanjara Nyeoja,alisema wamefikia hatua hiyo kutokana na mchango mkubwa unaotolewa na mbunge huyo katika sekta ya elimu hasa kwa kujenga shule nzuri na za kisasa zikiwemo nyumba za walimu katika jimbo hilo.

Aidha alisema bado sekta ya elimu imekuwa ikikabiliwa na changamoto lukuki zinazowakabili  shule za msingi na sekondari likiwemo tatizo kubwa la ukosefu wa nyumba za walimu.

“Walimu hususani maeneo mengi ya vijijini walimu wetu wanafundisha katika mazingira magumu kwa kukosa nyumba za kuishi hata kufikia walimu wengi kufikia hatua za kuhama wilaya yetu na kusababisha upungufu mkubwa wa walimu na wanaobaki sasa wazidiwa kazi ya kufundisha watoto wetu”alisema Nyeoja.

Hata hivyo katibu huyo wa cwt,aliomba mbunge huyo kusaidia uanzishaji wa SACCOS ya walimu wa wilaya hiyo ambayo itasadia kwa kiasi kikubwa kuwapunguzia makali ya maisha yanawakabili walimu.

Kwa sababu hiyo,walimpongeza mbunge huyo kuonyesha mfano mkubwa wa kutumia raslimali zake kwaajili ya kujenga vyumba vya madarasa katika shule za msingi na sekondari zikiwemo nyumba za walimu katika jimbo hilo.