Monday, November 19, 2012

RC AAGIZA MAZAO YAFYEKWE ILI KUNUSURU MIGOGORO TARIME *asema mipaka ionyeshwe vizuri *wananchi wataka Serikali kuwekeza eneo hilo


   Mkuu wa mkoa wa Mara Bw John Tuppa akisoma ramani na baadhi ya maafisa wilayani Tarime

 

KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA MKOA WA MARA,IMELIAGIZA JESHI LA KUJENGA TAIFA JKT KWA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI,KUTEKETEZA MAZAO YOTE AMBAYO YAMEPANDWA KATIKA MASHAMBA YENYE UKUBWA WA HEKTA 193.3 IKIWA NI NJIA MOJA WAPO YA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI KATIKA KATA MBILI ZA WILAYANI TARIME.

SERIKALI LITWAA ENEO HILO MIAKA KADHAA ILIYOPITA BAADA YA KUGOMBANIWA NA WANANCHI KWAAJILI YA KILIMO JAMBO AMBALO LIMEKUWA LIKISABABISHA MAPIGANO  YA KOO YA MARA KWA MARA NA KUSABABISHA MAUJI YA WANANCHI.

MWENYEKITI WA KAMATI HIYO,AMBAYE PIA NI MKUU WA MKOA WA MARA BW JOHN GABRIEL TUPPA,AMETOA AGIZO HILO,BAADA YA KUTEMBELEA ENEO HILO NA KUKUTA LIKIWA LIMELIMWA MAZAO MBALIMBALI YAKIWEMO MAHINDI HATUA AMBAYO SASA IMEANZA KUONYESHA VIASHIRIA VYA KUTOKEA KWA MAPIGANO YA KOO ZA WANCHARI NA WAKIRA KUTOKA KATA ZA MWEMA NA NYAMARAGA KATIKA WILAYA HIYO YA TARIME.

AIDHA MKUU HUYO WA MKOA WA MARA,PAMOJA NA KUVIAGIZA VYOMBO HIVYO VYA ULINZI NA USALAMA KUYATAIFISHA NA KUYATEKETEZA MAZAO HAYO PIA AMEAGIZA KUKAMATWA WATU AMBAO WANAHUSIKA KUFYEKA ZAIDI YA EKARI 100 ZA MAZAO MBALIMBALI MASHAMBANI PAMOJA NA KUSABABISHA KIFO CHA ROBERT CHACHA MARWA AMBAYE ALIFARIKI BAADA YA KUKATWAKATWA NA MAPANGA AKIWA SHAMBANI

KWA MUJIBU WA MKUU WA MKOA WA MARA,ENEO HILO SASA LITAKUWA CHINI UANGALIZI WA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWAAJILI YA SHUGHULI MBALIMBALI ZITAKAZOPANGWA NA JESHI HILO KUANZIA SASA,HUKU VIONGOZI NA WATENDAJI WA WILAYA NA MKOA WAKIAGIZWA KUPIMA UPYA MIPAKA YA VIJIJI HIVYO.

No comments:

Post a Comment